![]() |
| Kipa wa Man United David De Gea. |
Mwangi K.Githinji.
David de Gea amepuzilia
mbali madai kwamba alihusika katika kesi ya ngono huku akisisitiza kuwa
atasalia na timu ya Uhispania kwenye michuano ya yuro.
Tuhuma hizo
ziliibuliwa hii leo zikiwa zimesalia siku tatu tu kabla ya kuanza kampeni ya taifa
la Uhispania kwa mechi dhidi ya Czech Republic.
Katika ripoti ya
polisi shahidi mmoja aliye chini ya ulinzi mkali anayedai kwamba alilazimishwa
kushiriki tendo la ndoa bila hiari yake kwenye hoteli mmoja iliyoko mjini
Madrid iliyokodishwa na Allende Fernandez hali maarufu Torbe aliye korokoroni
na ambaye kwa kuhusika na filamu za ngono.
Japo De Gea anaelezewa
kutokuwepo katika eneo la tukio shahidii huyo amedhibitisha kwamba kipa huyo wa
Manchester United alihusika kuandaa
mkutano huo akishirikiana na Torbe.
Aidha mlinda lango
huyo ameeleza kuduwazwa na taarifa hizo alipofanya kikao na wanahabari.

No comments:
Post a Comment