Monday, 27 June 2016

MESSI ATANGAZA KUSTAAFU.

Mchezaji Messi.
Na Mwangi K .Githnji.
Nyota wa timu ya Argentina na klabu cha Barcelona Lionel Messi ametangaza kuwa amestaafu soka la kimataifa baada ya timu yake ya Argentina kulazwa na Chile kwenye fainali ya Copa America .
Messi mwenye umri wa miaka 29 ameeleza kuwa alilazimika kuacha kulichezea taifa lake kwani ameshindwa kulisaidia kutwaa taji lolote.
Alikiri kuwa ilimuuma sana hasa ikizingatiwa kuwa ameambulia patupu tangia alipoanza kuiwakirisha Argentina mnamo mwaka wa 2005.
Ilikuwa ni mara ya nne kwa mchezaji huyo aliyeichezea Argentina mechi 112 kupoteza katika awamu ya fainali.


No comments: