![]() |
| Sajili mpya wa United Eric Bertrand Bailly. |
Mwangi K. Githinji.
Klabu
cha Manchester United kimekamilisha usajili wa mlinzi Eric Bertrand Bailly kutoka
Villarreal ya Uhispania ,japo bado hajapata stakabadhi zinazomruhusu kuichezea
United.
Bailly
amejiunga na United kwa mkataba wa miaka minne baada ya kufanyiwa vipimo vya
afya hii leo.
Mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 22, aliichezea Villarreal mara 47 msimu jana tangia alipohamia klabu hicho
mnamo mwaka wa 2015.
Kwa upande mwingine
ameweza pia kuichezea Ivory Coast katika mechi 15 na alikuwa kwenye kikosi
kilichotwaa kombe la mabara ya Afika mwaka wa 2015.

No comments:
Post a Comment