Thursday, 16 June 2016

PEDRO AWAZIA KURUDI BARCELONA.




 
Mchezaji wa Chelsea Pedro.
 Mwangi K. Githinji.
Staa wa Chelsea Pedro Rodriguez amekiri kuwa angetaka kurejea tena katika klabu cha Barcelona baada ya kufanya mazungumzo na Rais wao kuhusu  uwezekano wake wa kurudi Camp Nou.
Pedro amefichua alivyotamaushwa na kughura kwake kutoka Barca japo amefichua kwamba hakuwa na budi kwa kuwa alikuwa anataka kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
Akiwa na wanacatalunha hao winga huyo mwenye umri wa miaka 29 alifunga mabao 48 na aliibuliwa kutoka kwa timu yao ya chipukizi.
Iwapo ataondoka itakuwa ni pigo kwa mkufunzi mpya Antonio Conte ambaye anatarakiwa kutua Stamford Bridge baada ya michezo ya yuro ili kukinoa klabu hicho cha nchini uingereza.

No comments: