Thursday, 23 June 2016

POGBA AMEFANYA MAZUNGUMZO NA LIVERPOOL!

Mchezaji wa Juventus Paul Pogba.
Na Mwangi K. Githinji.

Ajenti wa nyota Paul Pogba  amekiri kuwa amefanya mazungumzo na klabu cha Liverpool.

Katika mechi 178 alizoichezea Juventus Pogba mwenye umri wa miaka 23 amewafungia mabao 34 baada yake kughuria Serie A akutoka Manchester united mnamo mwaka wa 2012.

Mino Raiola amesema kuwa amefanya pia mazungumzo na vilabu kadhaa vya uingereza na kile cha Real Madrid ambacho kinasemekana kuwa karibu kutwaa sahihi yake.

Mchezaji huyo ana dhamana ya yuro milioni 123 japo huenda ikawa vigumu kwa Liverpool kumnunua kutokana na ushindani mkali kutoka kwa united na Madrid.


No comments: