Thursday, 23 June 2016

RAMSEY KUFUFUA MZOZO WA MOURINHO NA WENGER .

Aaron Ramsey wa Arsenal.
Na Mwangi K .Githinji.

Meneja mpya wa Manchester United Jose Mourinho huenda akafufua mzozo wake na Arsene Wenger tena baada ya habari kuibuka kuwa anapanga kumsajili mchezaji Aaron Ramsey.

Kwa sasa kocha huyo wa kutoka Ureno anafanya juhudi kukiongezea nguvu kikosi  chake kabla ya kuanza kwa msimu ujao.

Ramsey ameonyesha viwango vizuri vya mchezo  akiwa na taifa lake la wales nchini ufaransa huku aklisaidia kumaliza kwenye nafasi ya kwanza katika kundi lao la B mbele ya Uingereza.



No comments: