![]() |
| Mchezaji Zlatan Ibrahimovic. |
Mwangi K. Githinji.
Nyota wa Sweden Zlatan Ibrahimovic amedhibitisha
kuwa atajiunga na klabu cha Manchester United kwenye majira haya ya joto.
Mshambuliaji huyo alichapisha ujumbe kwenye akaunti
yake ya mtandao wa kijamii ambapo alifichua habari hizo masaa machache tu baada ya united kuratibu
mechi ya matayarisho ya msimu ujao nchini Sweden.
Lakini bado staa huyo mwenye umri wa miaka 34
hajasaini mkataba wowote na miamba hao wa uingereza ambapo anatarajiwa kufanyiwa
vipimo vya afya wiki ijayo.
Zlatan amewahi kufanya kazi tena na Mourinho
walipokuwa klabuni cha Inter Milan na ataungana na sajili mpya wa mashetani hao
wekundu Eric Bailly.


No comments:
Post a Comment