Friday, 8 July 2016

ARSENAL ILIFAA KUSHINDA LIGI-PETER CECH.

Mlinda lango wa Arsenal Cech.
Na Mwangi K.Githinji.

Mchezaji wa Arsenal    Peter Czech amekiri kutamaushwa na msimu wake wa kwanza na miamba hao baada ya klabu hicho kuambulia bila taji lolote msimu jana.
Nahodha huyo alihamia Arsenal kutoka Chelsea kwa kima cha yuro milioni 11 kutokana na ushindani mkali kutoka kwa kipa mwenzake Thibaut Courtois.
Na japo wanabunduki hao walianza vizuri msimu kwa kushinda taji la community Shield baadaye walishindwa kufana kwenye ligi kuu ya uingereza.

Amesema kuwa mwanzoni walidhani kuwa walikuwa na kikosi bora ambacho waliamini kingepigania taji la ligi lakini hatimaye Leicester  wakawapiku na hivyo kulishinda.

No comments: