Tuesday, 5 July 2016

LUIS NANI AJIUNGA NA VALENCIA RASMI.

Mchezaji Luis Nani yuko nchini ufaransa na timu yake ya ureno.
Na Mwangi K. Githinji.

Klabu cha Valencia kimedhibitisha kuwa kimemsajili aliyekuwa winga wa Manchester United Luis Nani kutoka Fenerbahce.
Valencia wamemtwaa kwa kima cha yuro milioni 8.5 ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu.
Akiwa Fenerbahce alicheza mechi 46 huku akiwafungia mabao 12 msimu mzima.
Kwa sasa Nani yuko nchini Ufaransa ambapo analiwakilisha taifa lake la ureno kwenye mashindano yanayoendelea ya yuro wakiwa wameratibiwa kuchuana na Wales katika awamu ya nusu fainali.
Licha ya sahihi yake kuwaniwa na vilabu kadhaa vya uingereza ikiwamo Stoke City na Everton amefanya uamuzi wa kuhamia Valencia ambao wanashiriki ligi ya uhispania.


No comments: