![]() |
| Shisha ambayo pia hujulikana kama hookah hutumiwa sana Uarabuni na bara Asia. |
Ben Kirui
Serikali ya
Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa shisha nchini humo na kulitaka jeshi la
polisi kufanya kila juhudi kutokomeza uraibu huo.
Waziri mkuu
wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo na kusema uvutaji shisha umekuwa ukichangia
katika kudorora kwa maadili miongoni mwa vijana, na kuwapunguzia uwezo wa
kiakili na kimwili wa kufanya kazi.
Majaliwa
amesema watakaokaidi agizo hilo pamoja na wauzaji wa vilevi hivyo, wataadhibiwa
vikali.
Awali, Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikuwa ametangaza kuwa ni marufuku watu
kuvuta shisha hadharani iwe ni katika baa, klabu au eneo lolote la starehe.

No comments:
Post a Comment