![]() |
| Kutoka kulia: Mwendazake wakili Willie Kimani, mteja wake Josphat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri |
Ben Kirui
Maafisa wa
upelelezi kutoka marekani FBI watasaidia katika uchunguzi wa mauwaji ya wakili Willie
Kimani, mteja wake Josphat Mwendwa na dereva wa teksi Joseph Muiruri.
Mkurugenzi
wa CID Ndegwa Muhoro amehakikishia mahakama kwamba uchunguzi wa mauwaji hayo utakamilika
kwa siku 14 zijazo.
Hata hivyo
wakili wa chama cha mawakili nchini LSK Charles Kanjama amesema ripoti hiyo ya
Muhoro haina msingi huku akitaka wapewe nafasi ya kumuuliza maswali.
Wakati huo
huo afisa wa polisi Leonard Mwangi alifikishwa mahakamani na kuwekwa rumande
kwa muda wa siku 13 ili kuwapa polisi kukamilisha uchunguzi.

No comments:
Post a Comment