Tuesday, 25 October 2016

AMUUA MKEWE NA WANAWE KISHA AJITIA KITANZI

Joseph Muthaiga chifu wa eneo la Makuyu.

Robert Mwangi
Polisi katika kaunti ya Vihiga wameanzisha msako wa mwanamume mmoja ambaye anadaiwa kumuua mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka minane kwa tuhuma za kuiba shillingi 1000
Inadaiwa kwamba Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 45 kutoka kijiji cha Mwiitoko alimchapa mwanawe hadi akafa baada ya pesa alizopata kutokana na kuuza kuku kutoweka.
Kule Maragwa katika kaunti ya Muranga mwanamume mmoja amemuua mkewe pamoja na wanawe wawili kwa kile kinachokisiwa kuwa mzozo wa kifamilia.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 30 alitumiwa panga kutekeleza unyama huo na kisha kujitia kitanzi. Chifu wa eneo hilo amesema kuwa tukio hilo limeripotiwa kwa polisi ili uchunguzi uanzishwe.

No comments: