![]() |
| Naibu rais William Ruto atamwakilisha rais katika mkutano huo wa Angola. |
Ben Kirui
Rais
Uhuru Kenyatta amefutilia mbali ziara yake rasmi ya Angola kutokana na
shambulizi la kigaidi lililotokea katika eneo la Mandera usiku wa Jumatatu
ambapo watu 12 waliuawa.
Kupitia kwa msemaji wa ikulu Manoah Esipisu, rais amefutilia
mbali ziara hiyo ili kukabiliana na shambulio hilo na kuomboleza na familia
zilizopoteza wapendwa wao.
Aidha Rais amewahimiza wakenya kuungana pamoja na kushirikiana
na walinda usalama kwenye vita dhidi ya ugaidi.
Naibu rais William Ruto sasa ndiye atakayemwakilisha rais katika
mkutano huo wa Angola.
Wakati huo huo viongozi kutoka kaunti
ya Mandera wamelaani shambulio hilo la kigaidi huku wakisema ufisadi ndio
chanzo cha kikithiri kwa uovu huo.
Wakiongozwa na Seneta wa kaunti hiyo Billow Kerrow, wabunge
hao wamelaumu Serikali kwa kushindwa kuchukulia suala la usalama wa eneo hilo
kwa uzito.
Aidha Seneta huyo amesema utovu wa usalama katika kaunti ya
Mandera umeathiri shughuli za maendeleo katika eneo hilo kwani watu wasio
wenyeji ndio wamekuwa wakilengwa.

No comments:
Post a Comment