![]() |
Eric
Dier akimsogelea Ander Herrera baada ya tukio hilo (Picha: Getty)
|
KAPEDO JNR
Kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza almaarufu “the
three lions” muite Eric Dier, amesema kuwa atalipiza kisasi dhidi ya
mchezaji Ander Herrera, dakika tano kabla ya mechi hio kukamilika, mechi ambayo
Uingereza ilitoka sare ya kufungana magoli mawili kwa mawili dhidi ya Uhispania
hapo jana usiku.
Dier, ambaye ana miaka ishirini na mbili alisema, “nafikiri ni
wazi kwamba alinipiga kumbo, sababu nahisi maumivu kwa shavu langu, kwa hivyo
najua alivyofanya, na sikupendezwa na kitendo hicho”
Aidha Dier aliongezea kuwa, “Sina shida na watu kupigana mateke
wakati mwingine lakini hicho ni kitendo cha unyama na hakistahili”
Manchester United itaialika Tottenham Hotspurs ugani Old
Trafford kwenye mechi ya kuwania kombe la EPL tarehe 11 Disemba 2016

No comments:
Post a Comment