Thursday, 10 November 2016

IBRA AFICHUA MIPANGO YA KARIOBANGI SHARKS


KAPEDO JNR

Mshambulizi wa klabu ya Kariobangi Sharks Ibrahim Kitawi amefichua kuwa timu hio inapanga kuhifadhi alama zote za mechi zinazosalia kwa kuepuka makosa modogo ili kuongeza matumaini yao ya kupanda kwenye ligi kuu humu nchini KPL

Sharks wameandikisha matokeo ya kufana tangu walipotoka sare ya kutofungana dhidi ya Nakumatt tarehe 24 Oktoba 2016, huku wakijitahidi kuandikisha matokea mazuri kwa mechi zilizosalia jambo ambalo limewapelekea kupanda hadi nafasi ya pili  kwenye jedwali la ligi kuu nchini KPL.

Kitawi ameifungia Sharks mabao sita kwenye michuano minne ya hivi karibuni huku akisalia mfungaji bora wa klabu hio msimu huu akiwa na mabao kumi na mbili.
Oserian itaialika Sharks kwenye mechi ya kuwania kombe la Supa League ambayo imeratibiwa kuchezwa jumaapili hii tarehe 14 Novemba 2016

No comments: