![]() |
| Kundi la wakulima katika kaunti ya Laikipia. |
Na Mwangi K.Githinji
Wakulima kutoka maeneo ya Ng’arua na Kinamba kwenye
kaunti ya Laikipia wametoa wito kwa serikali ya taifa kuleta huduma za bodi ya
mazao na nafaka karibu nao.
Wakulima hao wamelalamikia kupunjwa na wanunuzi
ambao wamedai hununua mazao yao kwa bei duni jambo ambalo wanahisi kuwa
linaweza likarekebishwa ikiwa serikali italeta bodi hiyo katika eneo hilo.
Aidha wamesema kuwa ikiwa serikali itatilia maanani suala
hilo basi itakuwa ni afueni kubwa kwao kwa sababu wanahisi kana kwamba bei za
chini kwa mavuno yao zinakandamiza na kuhujumu juhudi zao kama wakulima.

No comments:
Post a Comment