Thursday, 10 November 2016

JENGO LAPOROMOKA HUKO KISII NA KUUA.

Vifusi vya jengo lililoporomoka
Robert Mwangi

Jumba la orofa tisa ambalo ujenzi wake ulikuwa ungali  unaendelea liliporomoka huko Kisii na kuleta maafa ya watu sita akiwemo mtoto wa miaka kumi na mitano.

Wananchi waliofika eneo  la mkasa walitatiza pakubwa shughuli  ya ukoaji  iliyokuwa ikiendeshwa na shirika la msalaba mwekundu chini ya ulinzi wa polisi.

Zaidi ya watu arubaini wameokolewa na mashirika ya uokoaji huku mashirika hayo yakiendelea na shughuli ya ukoaji wakisema kuwa wana matumaini kuwa wataweza kupata watu zaidi wakiwa uhai.


Ujenzi  wa jumba hilo umekosolewa na wengi hasa ikizingatiwa kuwa halmashauri ya ujenzi wa manyumba ilikuwa imeharamishwa ujenzi wa jumba hilo kama  alivyokiri fundi mmoja aliyekuwa akishiriki ujenzi wa jumba hilo.

No comments: