Kiungo wa
zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na miamba wa ligi kuu ya Uingereza Chelsea, muite Frank
Lampard ataigura klabu hiyo mwezi ujao, Disemba
Mnamo jumaatatu kupitia kwa
mtandao wao (www.nycfc.com), klabu hiyo ilitangaza
kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 ataihama klabu hiyo baada ya mkataba
wake kukamilika mwisho wa mwaka huu, 2016
Lampard
alisajiliwa na klabu ya New York mwaka wa 2014, huku akitia wavuni magoli 15
kwenye mechi 31 alizochezea klabu hiyo.
Lampard alinukuliwa akiwashukuru
mashabaiki wa klabu hiyo kwa uungwaji mkono na ukarimu wao waliodhihirisha kwa
klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita

No comments:
Post a Comment