![]() | |
A Pregnant Woman |
Mwanamke wa Uganda ambaye anafanya kazi nchini Kuwait amehukumiwa kifungo cha miaka 5 pamoja na mwanawe kwa kosa la kushika mimba nje ya ndoa.
Nambi Fatumah alifikishwa mahakamani miezi kadhaa
iliyopita na kushtakiwa kwa kosa hilo.
Kulingana na
mwenyekiti wa chama cha Waganda wanaoishi nchi za bara Asia, Ali Nusbuga, Fatuma angeokolewa ikiwa serikali
ya Uganda na mashirika ya haki kwa binadamu yangeingilia kati.
Nchini Kuwait, mwanamke hafai kupata
mtoto kabla ya kuolewa ama nje ya ndoa na yeyote anayekiuka sharia hii, yeye
hufungwa jela bila kujali dini, rangi wala alikotoka.
Nusbuga
anaiomba serikali ya Uganda kuingilia suala hili na kutumia diplomasia ili
kumrejesha nyumbani Fatumah au hata kumpunguzia kifungo hicho. #Asante.
No comments:
Post a Comment