![]() |
Kinara wa Cord Raila Odinga na Rais wa jamhuri yaKenya Uhuru Kenyatta |
Kinara wa Cord angali ameshikilia msimamo wake kuwa shilingi
billioni 140 za hawala ya EuroBond hazijulikani zilipo.
Odinga alisema haya wakati wa mahojiano katika kituo kimoja cha
talevisheni hapa nchini, huku akidai kuwa serikali imekuwa ikicheza kayaya za
chini kwa chini, kuhusu vile ambavyo imechukulia swala la EuroBond ,waama
hesabu zenyewe haziafikiani, hivyo kuwaacha wakenya na maswali mengi kuliko
majibu.
Kiongozi huyu amekuwa mpiga filimbi kwenye swala hilo kwa miezi
kadhaa iliyopita ,na kusema kuwa taarifa za benki zilizotolewa na serikali
kutoka benki ya JP Morgan ,sio kamilifu na kuwa zimeacha maswali mengi vile
vile mianya mingi.
No comments:
Post a Comment