Ada ya mkokoteni
Naivasha, Jumanne 14 Octoba 2014 Njonge Moses ECN Radio
Naivasha, Jumanne 14 Octoba 2014 Njonge Moses ECN Radio
Waendesha mikokoteni watatozwa 1200 kila mwaka
Waendeshaji wa mkokoteni pamoja na magari ya punda wataendelea
kutozwa shilingi 1200 kila mwaka la sivyo watozwe faini ya shilingi
5000 kulingana na kiongozi wa kamati inayokusanya ushuru mjini
Naivasha Bw Genson Sifuna.
Sifuna alisema kuwa hata kama lengo lao ni kukusanya shilingi 3000 kwa
mwaka, wataendelea kukusanya 1200 kabla yao kukubaliana na
wanabiashara hao.
Akizungumza katika jumba la mikutano la manispaa ya mji wa Naivasha
alipokuwa amekutana wanabiashara hao, Sifuna aliwaomba pia waziheshimu
sheria za barabarani ili wasitatize shughuli za usafiri ndani na nje
ya mji huo.
“Hakikisha umezifahamu sheria za barabara na uziheshimu kwa sababu
ukizikiuka, tutakupigia hatua kama sheria inavyotupasa” alisema Sifuna
Kwa upande wake, Alfred Owino ambaye ndiye naibu katika kamati hiyo,
alisema kuwa ni sharti kila gari la punda pamoja na mkokoteni
lisajiriwe upya katika ofisi yake.
“Tunatengeneza nambari mpya za usajiri na kila gari la punda au
mkokoteni lazime lisajiriwe ilikuweza kulitambua kwa urahisi ikiwa
mwenyewe atakiuaka sheria barabarani,” Owino alidokeza.
Halikadhalika, Owino aliongeza kuwa wanabiashara hao wanafaa
kuyaheshimu masaa wanayopaswa kuwa barabarani haswaa nyakati za
asubuhi na jioni.
Owino alisisitiza kuwa asubuhi waendesha magari ya punda wanafaa
kuanza kazi saa kumi na mbili na kumaliza saa moja unusu huku jioni
wakianza saa kumi na moja hadi saa kumi na mbili unusu katika barabara
ya Moi na ile ya Kenyatta kuashiria kuwa mchana hawafai kuwa katika
barabara hizo mbili kuu.
Hata hivyo, wanabiashara hao walionyesha kutoridhika kwao kupitia
mwenyekiti wao Joseph Thendu kuhusiana na masaa wanayofaa kuwa kazini
lakini wakahakikishiwa malalamishi yao yatatiliwa maanani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment