Kiungo wa Manchester United Bastian
Schweinsteiger yupo hatarini kufungiwa Mechi 3 za ligi kuu ya England baada ya
kufunguliwa Mashitaka na Chama cha Soka cha England FA , kwa kosa la Kinidhamu.
Schweinsteiger, mwenye Miaka 31,
anadaiwa kumpiga Beki wa West Ham Winston Reid kwa Mkono wa Kushoto walipokuwa
wakigombea Mpira wa Frikiki katika Dakika ya 40 kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England iliyomalizika 0-0 Jumamosi iliyopita.
Schweinsteiger amepewa hadi Alhamisi
Saa 9 Mchana kukana au kukubali Mashitaka.
Refa wa Mechi hiyo, Mark
Clattenburg, hakulitaja tukio hilo lakini aliongea na Wachezaji wote Wawili
baada ya tukio lenyewe.
Katika Taarifa yao, FA imesema kuwa
tukio hilo lilipitiwa na Marefa Watatu tofauti ambao kila mmoja aliafiki
lilistahili Kadi Nyekundu na ndio maana wakafungua Mashitaka dhidi ya
Schweinsteiger.
Ikiwa Schweinsteiger atafungiwa
Mechi 3 atazikosa Mechi za Ligi dhidi ya Bournemouth, Norwich City na Stoke
City na kurejea kwenye Mechi na Chelsea.

No comments:
Post a Comment