Na Lawrence Muyela
![]() |
| Beki wa Manchester United Chris smaling akimkabili Sanchez |
Manchester United wameondolewa
kutoka kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kushindwa na klabu ya
Wolfsburg kutoka Ujerumani Jumanne usiku.
Vijana hao wa Old Trafford waliondoka
Ujerumani na kichapo cha 3-2.
Red Devils walikuwa wameanza vyema
Anthony Martial alipowafungia baada ya kupata pasi kutoka kwa Juan Mata.
Lakini wenyeji wao Wolfsburg
walikomboa dakika tatu baadaye kupitia Naldo kisha wakajiweka kifua mbele
kupitia Vieirinha.
United walidhani wangesonga mbele
baada ya Josuha Guilavogui kujifunga lakini mwishowe wakajipata wametumwa
Europa League baada ya Naldo kufunga kwa kichwa dakika za mwisho.
Vijana hao wa Louis van Gaal
walijuwa wangefuzu kwa hatua ya 16 bora iwapo wangelaza Wolfsburg, au wafikie
matokeo ya PSV Eindhoven waliokuwa wakicheza dhidi ya CSKA Moscow.PSV waliibuka
na ushindi wa 2-1 na kuwaeka nje vigogo hawa wa uingereza.

No comments:
Post a Comment