Friday, 11 December 2015

Je, Daddy Owen Alimlaghai Denno??



Na KakaMusa.



 Baada ya kuachia collabo ya MBONA ambayo itasalia favorite kwa masikio ya wengi, DADDY OWEN  inadaiwa kuwa alimlipa DENNO shilingi milioni 1.
Denno, Bahati na Daddy Owen

Licha ya hayo, msanii BAHATI amesema kuwa DENNO amekuwa akiishi maisha ya umaskini na huenda alilaghaiwa na hakupewa pesa hizo. 

Hata hivyo, DADDY OWEN amejitokeza kinoma na kukanusha kuwa alimtumia DENNO kujifaidi mwenyewe.

“Nimeona watu wanatupiana maneno online lakini kama mtu mzima nimeona bora niende niongee na DENNO na familia kuhusu hili suala. Nimekuwa kwenye industry kwa miaka na siwezi hold grudges na mtu juu najua haya mambo huufanyika.” amesema DADDY OWEN.

Juzi DENNO na BAHATI waliachia kibao kinaitwa STORY YANGU ambacho kinaonyesha ni kama DENNO anateseka kisha BAHATI anamsaidia.

No comments: