![]() |
| Jaji mkuu Willy Mutunga |
Makamishna hao wakiongozwa na Philip Kinusu wameapishwa kufuatia kujiuzulu kwa aliekuwa mwenyekiti Mumo Matemu na kundi lake.
Wakizungumza kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika mahakama kuu, makamishna hao wameapa kukabiliana na ufisadi vilivyo.
Makamishna Jane Onsongo na Irene Keino waliondoka afisini mwezi machi na Aprili mwaka uliopita.
Rose Mghoi Mtambo Macharia, Dabar Maalim Abdi, Paul Mwaniki Gachoka na Sophia Lepuchirit ni Miongoni mwa walioapishwa.

No comments:
Post a Comment