Monday, 18 January 2016

WANAJESHI WALIOJERUHIWA EL ADE SOMALIA WAWASILI NCHINI

 Na Ben Kirui

Wanajeshi 14 waliookolewa kufuatia mapigano yalioshuhudiwa huko El Ade Somalia wamewasili nchini adhuhuri hii.
Waziri wa Ulinzi Rachael Omamo katika uwanja wa ndege wa Wilson
 Wanajeshi hao wamepokelewa na waziri wa ulinzi Rachel Omamo na mkuu wa majeshi Samson Mwathete.
Hata hivyo hamna aliyejeruhiwa kati ya 15 hao.Jeshi la Kenya linaendeleza oparesheni ya kuwasaka na kuwaokoa wanajeshi walioathirika na shambulizi la waasi wa Al shabaab katika eneo la El adde Somalia.
        Mkuu wa majeshi Samson Mwathethe anasema oparesheni hiyo  inaendeshwa kwa umakini ili kuzuia vifo zaidi vya wanajeshi wa Kenya.
 Aidha Waziri wa ulinzi Rachael Omamo amesema jamaa za waathiriwa wanaendelea kufahamishwa kuhusu wapendwa waliofariki wakati wa shambulizi hilo.
    Akiongeza kuwa wameanzisha vituo maalum vya kuwahudumia jamaa za waathiriwa katika kambi za kijeshi zilizoko Eldoret, Gil Gil na forces memorial hapa jijini Nairobi.

No comments: