![]() |
| Mwenyekiti wa NPSC na wanakamati wa Tume ya NPSC |
BEN KIRUI
Maafisa saba wa polisi wameachishwa
kazi na Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi NPSC baada ya
kufichuliwa kwamba walitumia vyeti ghushi wakati wa usajili wa polisi.
Utovu wa nidhamu wa afisa msimamizi
wa polisi wa kitengo cha utawala Nelson Omwega ilibainika leo wakati Tume ya
kitaifa ya huduma za polisi ilikuwa ikitangaza kutimuliwa kwa maafisa hao.
Aidha Tume hiyo imebaini kwamba vyeti vya afisa Nelson Omwega vinaonyesha kuwa alikuwa
katika darasa la nane akiwa na miaka kumi pekee.
Mwenyekiti wa NPSC Johnstone
kavuludi amesema kuwa maafisa ambao wametimuliwa walijihusisha na ufisadi,
utovu wa nidhamu, na ukiukaji wa haki za kibinadamu.

No comments:
Post a Comment