 |
| Kiongozi wa mashtaka Bi Fatou Bensouda |
BEN KIRUI
Upande wa mashtaka katika Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu (ICC) umedai kwamba NAIBU wa Rais William Ruto alilipa
vijana Sh500 kila mmoja kutekeleza ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.
Madai hayo ni miongoni mwa ufichuzi
wa kina zaidi kuhusu mashtaka yanayomkabili naibu wa rais, ambayo yalifichuliwa
jana na Kiongozi wa Mashtaka Bi Fatou Bensouda.
Kulingana na Bi Bensouda, pesa hizo
zilikuwa zinakabidhiwa na wawakilishi wa Bw Ruto, hasa mwandani wake Bw Farouq
Kibet, kwa vijana wakati wowote walipohudhuria mikutano ya kuandaa mashambulizi
dhidi ya jamii zilizoaminika kuwa wapinzani wa chama cha ODM katika uchaguzi
huo.
Kwenye nakala iliyotolewa
Jumatano hii, jambo jingine lililofichuliwa ni kuwa Gavana wa Bomet Isaac Ruto
alihudhuria mojawapo ya mikutano ambapo inadaiwa mipango ya vita iliandaliwa. |
No comments:
Post a Comment