![]() |
| Jaji mkuu Willy Mutunga |
Na Ben Kirui
Tume ya Huduma za Mahakama JSC imeteua jopo la maafisa 6
kuchunguza tuhuma za ulaji rushwa ya milioni 200 zinazomkabili jaji wa mahakama
ya juu Philip Tunoi.
Rais wa JSC Jaji mkuu Dkt Willy
Mutunga ametangaza hayo baada ya kikao maalum cha dharura kilichoitishwa
kufuatia hatua ya Bw Geoffrey Kiplagat kupasua mbarika kuwa yeye ndiye aliyefanikisha
hongo ya shiilingi millioni 200 kwa jaji Tunoi ili awashawishi wenzake
kupendelea upande mmoja wakati wa uamuzi wa kesi ya kupinga uchaguzi wa gavana wa
Nairobi Dkt Evans Kidero.
Jopo hilo linajumuisha mkuu wa
sheria Prof Githu Muigai, Mkuu wa tume ya utumishi wa umma Prof Margaret Kobia,
jaji Aggrey Muchelule, Bi Emily Ominde, Bi Winnie Guchu na Bw Kipkorir Bett.
Sita hao wanapaswa kukamilisha
uchunguzi huo na kutoa taarifa kwa tume ya JSC inayosimamia maswala ya haki na
mahakama nchini katika kipindi cha siku saba sijazo.
Aidha Jaji Phillip Tunoi na Gavana
Evans Kidero wamejitokeza wazi wazi na kukanusha tuhuma hizo.

No comments:
Post a Comment