By Lena Juliet
Wizara ya masuala ya ndani
imewasimamisha kazi kwa muda takriban maafisa mia moja kwa kushindwa kukabili
matumizi na biashara ya pombe haramu maeneo tofauti ya nchi.
Akiongea huko kiambu katibu katika
wizara hiyo Karanja Kibicho amesema kuwa manaibu wa chifu na machifu wataachishwa kazi iwapo maeneo yao
yataendelea kuendesha biashara hiyo.
Anasema maafisa hao wamekuwa
wakishirikiana na watengenezaji na wauzaji wa pombe hiyo. Amekosoa idara ya
mahakama kwa kukosa kutoa adhabu kali kwa wahusika.

No comments:
Post a Comment