Thursday, 3 March 2016

SAMBURU WADAI KUTENGWA NA TUME YA UCHAGUZI IEBC.



By Lena Juliet

Viongozi na wenyeji wa kaunti ya Samburu wameilaumu tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa kukosa kufikia maeneo yote ya kaunti hiyo katika zoezi linaloendelea kuwasajili wapiga kura.
Gavana wa Samburu Moses Lenolkulal anasema licha ya muda mfupi uliosalia makarani wa IEBC hawajafika katika baadhi ya vituo kaunti hiyo.
Nao wenyeji wameitaka srikal kuwatuma maafisa wa usajili wa watu katika maeneo ya mashinani ili kufikia wakaazi wanaotaka vitambulisho vya kitaifa.

No comments: