![]() |
| Mahakama ya Kimataifa ua Uhalifu (ICC) |
Ben Kirui
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC
imetishia kuchukulia Kenya hatua kali iwapo haitasalimisha kwa mahakama hiyo
washukiwa watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya kutatiza mashahidi.
Msemaji wa
ICC Fadi el Abdalla amesema mahakama hiyo itaripoti Kenya kwa baraza la mataifa
wanachama wa mkataba wa Roma iwapo serikali itashikilia msimamo wa rais Uhuru
Kenyatta wa kutowasilisha wakenya hao watatu mbele ya mahakama hiyo.
Kiongozi wa
mashataka wa ICC Fatou Bensouda tayari amepata kibali cha kuwakamata aliyekuwa
mwanahabari Walter Baraza, wakili Paul Gicheru na Philiph Bett kwa madai ya
kutatiza mashahidi katika kesi dhidi ya naibu Rais William Ruto na mwanahabari
Joshua Sang’.
Akihutubia hafla
ya maombi ya shukrani iliyofanyika katika uwanja wa Afraha mjini Nakuru siku ya
jumamosi baada ya kutamatishwa kwa kesi za wakenya kule ICC, rais Kenyatta alisema kuwa
hakuna mkenya yeyote ambaye atafikisha katika mahakama ya ICC kujibu mashtaka.

No comments:
Post a Comment