Wednesday, 13 April 2016

WAZIRI MKUU WA NAMIBIA MIONGONI MWA WATAKAOHUDHURIA KONGAMANO LA UGATUZI MERU

Waziri mkuu wa Namibia Saara Amadhila
Ben Kirui

Waziri mkuu wa Namibia Saara Amadhila anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la tatu la kila mwaka la ugatuzi litakaofanyika katika kaunti ya Meru wiki ijayo.

Naibu mwenyekiti wa baraza la magavana Salim Mvurya amesema magavana pamoja na viongozi wengine wanaalikwa.

Waziri wa ugatuzi na mipango Mwangi Kiunjuri naye amependekeza kuwepo kwa ushirikiano kwa magavana na taasisi nyingine za serikali ili kuhakikisha mfumo wa ugatuzi unafaulu nchini.


Rais Uhuru Kenyatta ambaye ni mgeni rasmi, naibu wake William Ruto ni miongoni mwa wageni elfu sita kutoka kila pembe ya nchi watakaohudhuria hafla hiyo.

No comments: