![]() |
| Sajili mpya wa Arsenal Granit Xhaka. |
Mwangi K. Githinji.
Mashabiki wameendelea
kuiponza klabu ya Arsenal pamoja na sajili wake mpya Granit Xhaka.
Hii ni baada ya staa
huyo kuibua madai kwamba yeye ni kiongozi, akirejelea tukio la awali ambapo
mamake alikuwa akimwachia funguo za nyumba alipokuwa mchanga, licha ya kuwa na
ndugu aliyemzidi umri.
Wengi kwenye mitandao
ya kijamii wamemkemea sana huku baadhi yao wakimtania na kumuambia kwamba
asidhani kuwa yeye ni kiongozi katika soka kwa sababu tu alipewa majukumu ya
kuweka funguo katika zama hizo za utotoni.
Licha ya hayo ni wazi
kuwa Xhaka aliyehama kutoka Borussia Monchengladbach ya ujerumani ni kiungo mzuri na ambaye atakiimarisha
kikosi cha wanabunduki hao.

No comments:
Post a Comment