Saturday, 28 May 2016

USIMAMIZI WA MASWALA YA WALIMU HAYAKUHUSU WEWE MATIANG'I, ASEMA SOSSION.

Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion
Na Ben Kirui

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion amemtaka waziri wa elimu Dkt Fred Mating’i kukoma kuingilia usimamizi wa maswala ya walimu.

Akizungumza huko Kericho Sossion amesema jaribio la serikali kutaka kumbandua uongozini halitafaulu kwa kuwa walimu tayari wamempa jukumu la kusimamia na kutetea maslahi yao kikamilifu.


Sossion aidha, amemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati mgogoro unaonukia kati yake na waziri wa elimu Fred Matiang’i. 

No comments: