![]() |
| Isco na mbwa wake anayeitwa Lionel Messi. |
Mwangi K. Githinji.
Staa wa Real Madrid Isco
amefichua kuwa mbwa wa familia yake anaitwa Lionel Messi ,sawia na nyota huyo
wa Barcelona.
Isco anayetoka nchini
Uhispania anadai kuwa Messi hakumchochea kumpa jina hilo, japo
alikubali kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Messi.
Kulingana na mchezaji
huyo wazo la kumpa jina hilo lilitoka kwa babake na kakake ila sio kwake.
Alisema mbya huyo yuko
na wazazi wake kwa sasa, huku akieleza kuwa ameacha kutembea naye
kwenye mitaa ya Madrid
kwa sababu ni kinaya kwake kumuita jina hilo mbele ya umma hasa ikikumbukwa
kwamba wengi wanaoishi huko ni mashabiki wa Real Madrid.
Hivyo basi anaogopa kuwa
huenda tendo hilo likaibua mgogoro baina yake na wafuasi
hao.

No comments:
Post a Comment