Thursday, 12 May 2016

MISA YA MFANYIBIASHARA JACOB JUMA YAFANYIKA

Mwendazake Jacob Juma
Ben Kirui

Misa ya wafu ya mfanyibiashara aliyeuawa wiki iliyopita inaendelea katika kanisa la All saints Cathedral hapa jijini Nairobi.

Kinara wa Cord Raila Odinga na kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi miongoni mwa viongozi wengine wanahudhuria misa hiyo.

Baada ya kukamilika kwa misa mwili wa Juma utapelekwa katika bustani ya Uhuru ambapo umma utaruhusiwa kuutazama.

Jacob Juma aliuawa na watu ambao hawajatambulika kwa kupigwa risasi kufikia Jumatano polisi walikuwa wakiendelea na uchunguzi kubainisha kifo hicho.

No comments: