Monday, 9 May 2016

WAFUASI WA CORD WAKAIDI AMRI YA SERIKALI NA KUANDAMANA HADI AFISI ZA IEBC


Cord waendeleza shinikizo za kutaka makamishna wa IEBC kung'atuka

 Ben Kirui

Wafuasi wa mrengo wa upinzani Cord wamekaidi amri ya serikali na kuandamana katika afisa za tume ya uchaguzi na maeneo mipaka nchini IEBC kushinikiza maafisa wa tume hiyo kujiuzulu.

Ilibidi maafisa wa polisi hapa jijini Nairobi kutumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji wa muungano wa Cord waliokuwa wameandamana hadi afisi za tume hiyo

Kiongozi wa Cord Raila Odinga anashikilia kuwa makamishna wa IEBC hawawezi kusimamia uchaguzi huru na wa haki mwaka ujao.

Hii ni mara ya pili kwa muungano huo kufanya maandamano hadi afizi za IEBC huku muungano huo ukishikilia kwamba wataendelea na shinikizo za kutaka makamishna wa IEBC kung'atuka.

No comments: