Thursday, 5 May 2016

WAPENZI WA JINSIA MOJA WAELEKEA MAHAKAMANI KUPINGA UKAGUZI WA 'TUPU YA NYUMA'



Wapenzi wa jinsia moja

 Ben Kirui

Wanaume wawili ambao wanasema waliwalazimisha  na maafisa wa polisi kufanyiwa ukaguzi wa tupu ya nyuma ili kubaini kwamba walishiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja wameanzisha kesi mahakamani wakitaka ukaguzi huo kuwa ukiukaji wa katiba.

Wanasema kuwa walilazimishwa kufanyiwa ukaguzi wa magonjwa ya virusi vya ukimwi na Hepatitis kufuatia kukamatwa kwao mnamo mwezi Februari 2015 baada ya kushukiwa kwamba wanashiriki katika ngono ya mapenzi ya jinsia moja.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja kushiriki ngono ni kinyume na sheria hapa nchini na adhabu ya makosa hayo ni kuhukumiwa miaka 14 gerezani.

Mahakama ya Mombasa imewapatia mawakili wa serikali wiki moja kutoa jibu.

1 comment:

Anonymous said...

TO HELL WITH THEM