Saturday, 28 May 2016

WAZITO FC WAWAZAMISHA SHABANA.


Wachezaji wa Wazito Fc wakisherehekea bao.
Na Mwangi K. Githinji.
Mechi za ligi ya daraja la kwanza ziliendelea hii leo ambapo Wazito FC waliwacharaza Shabana ambao wamo kwenye nafasi ya mwisho mabao 3-0 katika mechi iliyochezewa ugani wa Awendo Green Stadium.
Kabla ya mchezo huo Wazito walikuwa wamepoteza mechi zao tatu zilizopita huku nao Shabana wakiwa bado hawajashinda mechi yeyote hadi sasa.
Zoo Kericho nao waliwashinda KCB mabao 4-1 huko Kericho Green Stadium.
Katika maeneo ya Naivasha ,wenyeji  Oserian walilazimishwa kutoka sare ya kutofungana kwenye mchezo uliokuwa wa kusisimua japo timu zote mbili zilishindwa kuzitumia nafasi zao vizuri.


No comments: