![]() |
| Straika De Lima. |
Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Kenya Gor Mahia hawatamsajili straika Thiago De Lima anayetokea nchini Brazil na atakuwa anaondoka nchini hii leo jioni.
Mbrazili huyo alikuwa anafanya mazoezi na klabu hicho kwa kipindi wa wiki tatu huku akisubiri wampe kandarasi lakini sasa mwakilishi mmoja wa benchi la Gor la ufundi amejitokeza na kufichua kuwa mchezaji huyo hakumridhisha mkufunzi Ze Maria.
Gor wataingia sokoni kumtafuta mshambulizi mbadala ambapo inakisiwa kuwa wanafanya mazungumzo na Meddie Kagere ili wamsajili tena.
Kuondoka kwa De Lima kunawapa mashabiki wa klabu hicho kumbukumbu za mchezaji mwingine wa kutoka Brazil Geovanni Rodriguez ambaye pia alitemwa na miamba hao mnamo mwaka wa 2013 na mkufunzi Zdravko Logarusic.

No comments:
Post a Comment