Ajenti wa meneja wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc amefichua kuwa
mteja wake atakaghura miamba hao wa ufaransa katika siku chache zijazo.
Imeripotiwa kuwa PSG watamteua aliyekuwa mkufunzi wa Sevilla Unai Emery ili alijaze pengo hilo.
Akiwa na PSG aliwasaidia kushinda mataji kadhaa yakiwamo ya ligi kuu ya ufaransa japo kutokana na yeye kushindwa kupata mafanikio ya haja kwenye mashindano ya klabu bingwa ulaya miamba hao wamefanya uamuzi wa kumtema.
Kocha huyo ajiunga na PSG mnamo mwaka wa 2013 na kando na kuisaidia klabu hiyo kutwaa mataji pia aliwahi kuwa mkufunzi bora wa mwaka wa 2014/15.
Kwa upande wake Emery atakumbukwa hasa kwa kuiongoza timu yake
kulishinda kombe la yuropa mara tatu mtawalia.

No comments:
Post a Comment