Monday, 20 June 2016

PEDRO AOMBA MSAMAHA .

Mchezaji wa Uhispania na chelsea Pedro.
Na Mwangi K .Githinji.

Mchezaji wa Uhispania na klabu cha Chelsea Pedro Rodriguez ameomba  msamaha kufuatia kauli yake, alipokiri  kwamba hana furaha kwa kukosa kuchezeshwa kwenye michuano inayoendelea ya yuro na kuwa alikuwa anawazia kuondoka kutoka kwa michezo hiyo.

Winga huyo wa Chelsea aliingia kama nguvu mpya kwenye mechi yao ya kwanza na Czech Republic lakini akakosa kupewa nafasi Uhipania ilipokabiliana na Turkey hivi majuzi.


Licha ya haya kauli yake ilibadilika pindi tu alipofanya kikao na wanahabari hapo jana akisema kwamba tayari wamesuluhisha swala hilo na mkufunzi Del Bosque pamoja na wachezaji wenzake na kulizika kwenye kaburi la sahao.

No comments: