Sunday, 5 June 2016

GUORDIOLA AMA MOURINHO NANI ATAMTWAA AUBEMEYANG?

Mchezaji Pierre Emerick Aubemeyang
Vilabu vya Manchester United na Manchester City vimeingia kati vita vya mgao vinapoiwania sahihi ya mchezaji nyota wa klabu cha  Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang.
Straika huyo anayekisiwa kugharimu ada ya yuro milioni £65 amefana sana akiwa na miamba hao wa ujerumani msimu huu, ambapo amefaulu kutia kimiani jumla ya mabao 36.
Jose Mourinho na Pep Guardiola wanaripotiwa kuwinda sahihi yake licha yake kuwa na mkataba unaombakiza huko Westfalenstadion hadi mwaka wa  2020.
Kando na City na United Aubameyang pia amehusishwa na uhamisho wa kwenda Arsena na Real Madrid.



No comments: