Kigogo wa Brazil Pele ameibua madai
kuwa mchezaji Neymar da Silva bado hajafikia viwango vya mastaa Lionel Messi na
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Nyota huyo wa Barcelona alikuwa watatu nyuma ya mastaa hao
wawili katika tuzo za mwaka jana za Ballon d'Or na wengi wameeleza kuwa huenda
akaishia kuwa mchezaji bora zaidi duniani.
Japo
Pele amekuwa akimtaja Neymer kama mchezaji mzuri amekubali kuwa itamchukua muda
kufikia viwango vya Messi na Ronaldo akiongeza kuwa Messi ni ndiye mchezaji
bora zaidi kumshinda Ronaldo.
Neymar
kwa sasa hajajumuishwa kwenye kikosi cha Brazil kinachoshiriki mashindano ya
Copa Amerika lakini anatarajiwa kuwachezea kwenye michezo ya Olimpiki itakayofanyika
Rio de jeneiro
.

No comments:
Post a Comment