Baada ya mlinzi wa
Bayern Munich Jerome Boateng kuwakemea washambulizi wa timu hiyo kutokana na
sare yao ya 0-0 dhidi ya Poland, staa wa arsenal Mesut Ozil amejitokeza na
kumjibu.
Ujerumani waliambulia
sare ya 0-0 kwenye mechi hiyo ya awamu ya makundi jambo ambalo halikumfurahisha
mlinzi huyo akisema kuwa kitengo cha timu yao kilikosa maarifa ambayo
yangewasaidia kupenyeza safu ya ulinzi ya Poland.
Ozil amemnyamazisha
Boateng huku akimpa jibu la utani akimwambia kwamba usemi wake ni maoni tu na
kwamba ana ruhusa ya kunena maneno hayo kwa kuwa yeye ni fundi wa kucheza soka
la kushambulia.
Kwa sasa timu hiyo
inayofunzwa na kocha Joachim Low inaongoza kundi C na watakabiliana na Northern
Ireland katika mechi yao ya mwisho.

No comments:
Post a Comment