![]() |
| Polisi wameanzisha uchunguzi wa kisa hicho cha kutamausha |
Ben Kirui
Polisi
katika kaunti ya Nyamira wanachunguza kisa ambapo mwanaume mmoja na mkewe walipoteza
maisha eneo Mobamba baada ya kushambuliwa na genge la watu wasiojulikana.
Inadaiwa kwamba
genge hilo la takriban watu 200 liliingia katika Nyumba ya wawili hao usiku wa
kuamkia Jumapili na kuwalazimisha kunywa petroli kabla ya kuwateketeza.
Ocpd wa
Nyamira Ricoh Ngare amesema uchunguzi umeanzishwa hasa ikidaiwa kwamba tendo
hilo ni la kulipiza kisasi.
Inaarifiwa kwamba
wawili hao walihusika katika kutiwa mbaroni kwa mshukiwa mmoja wa wizi ambaye
alifariki baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani.

No comments:
Post a Comment