Arsene Wenger amefichua kwamba atanunua wachezaji watatu
pekee msimu huu wa majira ya joto kwa kuwa hataki kusababisha mtafaruku kwenye
kikosi chake kwa kuwanunua wachezaji wengi sana.
Tayari klabu chake kimekamilisha usajili wa nyota wa taifa la Switzerland Granit Xhaka japo Wenger amepuzilia mbali madai kuwa wamemsajili Jamie Vardy kutoka Leicester city .
Meneja huyo atakuwa anapania kutoa ushindini mkali ligini msimu ujao huku timu hiyo ikiwa imekwenda kipindi cha miaka 12 bila kutwaa taji la ligi kuu ya uingereza..
Arsenal wamewapoteza wachezaji Mikel Arteta,Tomas Rosicky na Mathieu Flamini na mkufunzi huyo amekiri kuwa sajili wapya watajaza nafasi zao.

No comments:
Post a Comment