![]() |
| Mkufunzi Tite. |
Aliyekuwa mkufunzi mkuu wa klabu cha Corinthians Tite ameteuliwa kama meneja mpya wa timu ya taifa ya Brazil.
Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 55 atachukua nafasi ya Dunga na atachukua hatamu baada ya michezo ya Rio Olympic inayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 20 itakapotamatika.
Tite amevifunza vilabu 13 ikiwamo Gremio, Atletico Mineiro na Palmeiras vya huko Brazil, huku akishinda kombe la Copa Libertadores mara mbili na lile la dunia mara moja.

No comments:
Post a Comment