Tuesday, 21 June 2016

ZLATAN ATANGAZA KUSTAAFU SOKA.




Straika Ibrahimovic.
Na Mwangi K. Githinji.
Hatimaye straika wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amefichua kwamba atastaafu soka la kimataifa baada ya kukamilika kwa dimba linaloendelea la yuro.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alidhibitisha habari hizo siku chache tu baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki mashindano ya Olimpiki ya mwezi wa Agosti.
Timu yake inajitayarisha kukabiliana na Ubelgiji siku ya kesho wakiwa wanapania kufuzu kwa mkondo wa 16 bora mechi ambayo lazima waishinde.
Ibrahimovic alichezea Sweden kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 2001 huku akiwachezea mechi 115 na kufunga 62.


No comments: